Medeama walikuwa na 4-3-3 lakini walikuwa wakienda kushambulia wanakuwa 4-2-3-1 kiungo mmoja anakuwa nyuma ya straika Jonathan Sowah ambaye kulia na kushoto ana mawinga wawili … nini ambacho walikuwa wame target Medeama ?
1: Walijua ndani Yanga wapo wengi ambao bila mpira Yanga walikuwa 5-3-2 ( Maxi Pacome na Aucho kwenye kiungo ) kwahiyo wao wakaamua kutumia space pembeni ya uwanja ipi hiyo ?
2: Wingbacks wa Yanga walikuwa wanawafuata zaidi fullbacks wa Medeama maana yake wanaacha space pembeni ya Outside CBs wa Yanga ambao Job na Bacca na ndio maana wingers wa Medema walikuwa wanapata 1v1 dhidi ya Job na Bacca … ambayo faida yake ?
3: Hapo Medeama wanakuwa wanafanya kwamba Bakari anabaki ndani peke yake dhidi ya Jonathan Sowah ambaye alionekana hatari sana
✍🏻Yanga kwenye muundo wa 5-3-2 bila mpira na 3-1-2- 4 wakiwa na mali
1: Wakiwa na mpira , wingbacks wanasogea juu zaidi kuwa katika mstari mmoja na Musonda + Mzize huku nyuma yao ni Pacome na Maxi wakati Aucho anabaki kwenye namba 6 kutengeneza muundo wa ulinzi na wale watatu wa nyuma kwa ajili ya kukabiliana na counter attacks
2: Nafikiri tatizo kubwa la Yanga haikuwa mfumo bali ilikuwa : Ufinyu wa level ya kiufundi ( Technical ability ) pamoja na Maamuzi sahihi ( decision making ) kivipi ?
3: Kiufundi : yani kasi ya utekelezaji jambo linaloendana na kusudio : mara kadhaa wachezaji wa Yanga wakifika mbele mpira haukai mguuni , pasi haifiki , dribbling inaondoka mguuni zaidi na kupoteza mpira :
4: Maamuzi ambayo sio sahihi : aina ya pasi , wapi pa kupiga , ukimbie eneo gani , hayakuwa sahihi kwa nyakati sahihi .
✍🏻Kitu ambacho Gamondi atafurahia sana ni wachezaji wake kutojificha , kucheza bila hofu , kujituma uwanjani , na kuonesha dhamira ya kushinda mechi badala ya kucheza kwa ajili ya sare
VYA KUZINGATIA:
1: Jonathan Sowah yule mtu aisee 🔥
2: Amoako fullback inamwaga maji 🔥
3: Kibabage ana overlap vizuri lakini mpira wa mwisho bado
4: Bacca muda wote yupo tayari kupambana 🔥
5: Aucho akiwa na mali anarahisisha pasi zake🔥
6: Pacome He is so good aisee 🔥
7: Mechi ya kasi , end to end football
Unaweza kusoma zaidi hapa