Mchezo wa kwanza wa Argentina nyumbani baada ya ushindi wao wa Kombe la Dunia 2022, ulimalizika kwa ushindi kwa mabao mawili ya dakika za mwisho dhidi ya Panama ambao uliwafanya mashabiki wa Estadio Monumental huko Buenos Aires watabasamu na kufurahia ushindi.
Panama hawakufanya mchezo kuwa rahisi kwa Argentina, lakini Thiago Almada hatimaye alifunga bao la kuvunja ngome kwa upande wa nyumbani na dakika 10 zilizobaki, akimalizia mchezo mpira wa adhabu ‘Free kick’ iliyopigwa na Lionel Messi na kugonga mwamba wa kushoto.
Messi amefunga bao lake la 800 katika soka lake la kulipwa, na kuweka mpira wavuni kwa mpira wa adhabu uliolenga lengo kwa usahihi baada ya kupiga mwamba mara mbili kwenye nguzo wakati wa mchezo.
Haikuwa rahisi kwa kikosi hicho cha mabingwa wa kombe la dunia 2022 kupata ushindi kutokana na ulinzi imara na uokoaji sahihi wa kipa Jose Guerra.
Lakini ubora wa wachezaji wa Argentina ulikua imara, na ndipo ‘Super Sub’ Almada, mchezaji machachari wa klabu yake ya Atlanta United akiifunga bao la kuongoza, na Messi akijitokeza tena katika jezi ya Argentina kumalizia msumari wa pili.
Kulikuwa na sherehe na muziki kabla ya mechi, na sherehe zilizidi baada ya kipenga cha mwisho, na kwa sasa itaendelea na mchezo mwingine huko Santiago del Estero kwa siku ya Jumanne dhidi ya Curacao aliyepangwa 86 katika viwango vya FIFA.
Mabao: ARG – Thiago Almada – dakika ya 79.
ARG – Lionel Messi – dakika ya 89.
Vikosi vilivyocheza:
Argentina (4-3-3, kulia kwenda kushoto): 23-E. Martinez (GK) – 26-Molina, 13-Romero, 19-Otamendi (25-Li. Martinez, 46′), 3-Tagliafico (8-Acuna, 66′) – 20-Mac Allister (16-Almada, 46′), 24-E. Fernandez (5-Paredes, 61′), 7-De Paul – 10-Messi, 9-J. Alvarez (22-La. Martinez, 46′), 11-Di Maria (21-Dybala, 61′).
Panama (5-4-1, kulia kwenda kushoto): 12-Guerra (GK) – 2-I. Anderson, 13-Ramos, 4-Farina (14-Hernandez, 65′), 5-Peralta, 3-Galvan (16-Casazola, 70′) – 19-Cordoba (20-Browne, 46′),